
Mamlaka za nchini Ureno zimemtia nguvuni na kumfungulia mashtaka mke wa rais wa Guinea-Bissau aliyepinduliwa, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya utakatishaji fedha. Hayo yameelezwa na polisi ya nchi hyo.
Dinisia Reis Embalo, mke wa Umaro Sissoco Embalo, aliwasili mjini Lisbon kwa ndege kutoka Guinea-Bissau sawa na abiria mwingine ambaye alikuwa amekamatwa siku ya Jumapili.
Taarifa ya Polisi ya Ureno imesema, abiria huyo alitiwa nguvuni na kukutwa na karibu yuro milioni tano ($5.9 milioni) fedha taslimu, na alishukiwa kuhusika na utakatishaji pesa.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ureno mshukiwa wa kwanza ambaye ametambuliwa kama Tito Gomes Fernandes, alikuwa mtu wa karibu wa Rais wa Guinea-Bissau aliyepinduliwa Embalo, ambaye alikimbia nchi baada ya jeshi kumuondoa madarakani katika mapinduzi ya Novemba 26.
Msemaji wa polisi ya Mahakama amevieleza vyombo vya habari bila kutoa ufafanuzi zaidi kwamba, mashtaka yanayomkabili Bi Dinisia Reis Embalo “yamehusishwa” na uchunguzi huo.
Imeelezwa kwamba, ndege iliyokuwa imewabeba wawili hao ilikuwa awali imeorodheshwa kuwa ya kijeshi na ilitarajiwa kuelekea katika mji wa kusini mwa Ureno wa Beja.
Hata hivyo, “baadaye ilibainika kuwa ndege hiyo na inapoelekea ni tofauti”, na ilivyotangazwa, polisi wamesema.../