
Haya yakiwa miongoni mwa mauzo makubwa zaidi ya silaha kwa kisiwa hicho kinachojitawala, huku Washington ikilenga kuzuia uwezekano wa uvamizi kutoka China. Mpango huo, ambao bado unahitaji idhini ya Bunge la Marekani, unajumuisha mifumo ya roketi ya HIMARS, mizinga, makombora ya kupambana na vifaru, ndege zisizo na rubani pamoja na vifaa vingine vya kijeshi.
Yanakuwa mauzo ya pili ya silaha kwa Taiwan tangu Rais Donald Trump kurejea madarakani Januari, baada ya mpango wa awali wa dola milioni 330 mwezi Novemba.
Katika muongo mmoja uliopita, Taiwan imeongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya ulinzi, huku China ikiendelea kuiongezea shinikizo la kijeshi, ikidai kisiwa hicho ni sehemu ya himaya yake. Serikali ya Taiwan imesema mpango huo unaonesha dhamira ya Marekani katika kulinda usalama wake.