
Kampuni ya kitaifa ya kusambaza ya umeme nchini Sudan imesema mashambulizi hayo ya leo ya RSF yamesababisha kukatika kwa umeme katika baadhi ya miji mikubwa ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Khartoum na Port Sudan. Abdel Rahim al-Amin, afisa katika jimbo la Port Sudan, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa, AFP kuwa umeme ulikatika kwenye eneo hilo tangu saa nane usiku.
Katika miezi ya hivi karibuni, wanamgambo wa RSF wamekuwa wakishutumiwa kwa kuyashambulia maeneo makubwa yanayodhibitiwa na jeshi kwa kutumia droni, kuilenga miundombinu ya kiraia na kusababisha kukatika kwa umeme, na hivyo kuwaathiri mamilioni ya watu.