
Erdogan pia alipongeza vyombo vya habari vya Uturuki kwa misimamo ya “kijasiri” katika kuangazia ukweli ya yale yanayofanyika Gaza.
“Huku mauaji ya halaiki yakitokea Gaza, vyombo vya habari vya Uturuki, hasa TRT na Anadolu, vimechukuwa hatua za kijasiri,” kiongozi huyo wa Uturuki alisema.
Akimpongeza mpiga picha wa Anadolu Ali Jadallah, Erdogan alisema: “Kinachoonekana kupitia upigaji picha wake siyo tu kinaonesha ukatili wa mauaji Gaza lakini pia upambanaji wa haki wa watu wa Palestina ili dunia ipate kuona.”
“Kaka yetu Ali, ambaye ameonesha mauaji ya kikatili ya halaiki Gaza na kuonesha kile ulimwengu unaosemekana kuwa wa kistaarabu ukweli, anafanya kazi kama mpiga picha wa Anadolu,” alisema.