
Kabla ya mkutano huo, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ametoa wito kwa nchi wanachama kuidhinisha matumizi ya mali hizo, akisema hatua hiyo itaongeza shinikizo kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin na kuonesha mshikamano wa Ulaya.
Hata hivyo, baadhi ya nchi zikiwemo Ubelgiji, ambako kunahifadhiwa sehemu kubwa ya mali hizo, zinaeleza wasiwasi wa kisheria na kifedha. Zinataka makubaliano ya pamoja yatakayohakikisha nchi zote zitawajibika endapo Urusi itashinda kesi mahakamani. Umoja wa Ulaya unaonya kuwa bila msaada wa kifedha, Ukraine inaweza kukosa fedha mapema mwaka ujao, jambo linalohatarisha usalama wa bara hilo.