Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salim, Madbouly amewaambia waandishi wa habari kwamba Misri itaendelea kuimarisha juhudi za kuhakikisha Lebanon inabaki mbali na mzozo na jirani yake Israel.

Ziara ya Madbouly mjini Beirut imefanyika wakati kamati inayosimamia utekelezaji wa usitishaji mapigano uliofadhiliwa na Marekani – uliomaliza vita kati ya Israel na Hezbollah mwaka mmoja uliopita – ilikuwa ikifanya mkutano mwingine leo.

Misri ambayo ilisaini mkataba wa amani na Israel mwaka 1979, imekuwa ikifanya kazi kwa miezi kadhaa kupunguza mvutano wa kikanda.

Ziara ya Waziri Mkuu Madbouly inafuatia safari kama hizo zilizofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri pamoja na mkuu wa idara ya ujasusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *