
Matamshi ya viongozi hao yanafuatia hatua ya Rais Donald Trump kumteua mjumbe maalamu wa Washington kwa ajili ya Greenland na kuendelea kushinikiza umuhimu wa Marekani kuchukua udhibiti wa kisiwa hicho cha bahari ya Aktiki.
Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen na mwenzake wa Greenland Jens-Frederik Nielsen, wamesema kwenye tamko la pamoja jana Jumatatu kuwa kisiwa hicho kamwe hakitokwenda mikononi mwa Marekani na kupuuzilia mbali hoja za Washington kuhusu suala la usalama.
Trump amesema mara kadhaa kwamba angetamani Marekani ikinyakue kisiwa hicho kwa sababu za kiusalama, matamshi ambayo mara zote yamezusha ukosoaji mkubwa kutoka kwa Denmark, iliyo mshirika wa Washington.