Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, tunafuatilia kwa karibu hatari na nyendo kwa umakini mkubwa.

Sambamba na kubainisha kwamba, vikosi vya kijeshi vya Iran daima vinajitahidi kuongeza utayari wake kukabiliana na tishio lolote, ikiwa ni pamoja na vita visivyo vya kawaida na vita visivyo rasmi, Meja Jenerali Hatami amesisitiza kuwa, tuko macho na tunafuatilia kwa karibu harakati zote za adui na tutatoa jibu kali wowote wa uvamizi wa aina yoyote.”

Meja Jenerali Hatami ameongeza kuwa, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, likiwa na azma thabiti, limeweka kila kitu kinachohitajika kukabiliana na maadui zake. Mafunzo yote na mazoezi ya jeshi yamefanywa kwa mujibu wa kanuni za kijeshi, hasa mfumo wa ulinzi, na yameandaliwa kwa njia halisi kwa ajili ya uwanja wa vita.

Aliongeza: Leo, jukumu la jeshi pia ni kulinda umoja wa kijiografia wa Iran ya Kiislamu na uhuru wa nchi, na sote tunajitahidi kutekeleza jukumu hili kwa njia bora zaidi.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran aidha amesisitiza umuhimu na hadhi maalum ya Vikosi vya Anga vya Jeshi, akisema: “Moja ya vitengo muhimu katika eneo la magharibi mwa nchi ni Vikosi vya Anga, ambavyo, kwa kutumia vifaa vingi vilivyopo, vimepewa jukumu la kusaidia aina zote za vitengo katika maeneo ya magharibi.”

Wakati huo huo, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa utawala wa Israel unatekeleza mashambulizi ya “kujidhuru” dhidi ya jumuiya za Wayahudi maeneo mbali mbali duniani ili kuchochea hofu ya chuki dhidi ya Wayahudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *