Wanachama hao sita walioachiwa walikuwa na mafungamano na Domingos Simoes Pereira, ambaye ni mkuu chama cha siasa cha PAIGC kilichoiongoza nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1974. Pereira mwenyewe bado yuko kizuizini tangu jeshi lilipofanya mapinduzi.

Baraza Tawala la Kijeshi la nchi hiyo limesema kuachiwa kwa wanasiasa hao 6 ni “ishara ya nia njema kuelekea kurejea kwa utawala wa kikatiba na kuheshimiwa kwa haki za binadamu”.

Jeshi la Guinea Bissau lilichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mnamo Novemba 26 na kuuangusha utawala wa Rais Umaro Sissoco Embalo ambaye hivi sasa amekimbilia uhamishoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *