KIGOMA; TAASISI zisizo za kiserikali mkoani Kigoma zimeomba fedha kwa wahisani ili kusaidia jamii zenye uhitaji zimetakiwa kuhakikisha misaada ya fedha na vitu mbalimbali vinavyoombwa vinawafikia wahitaji.
Kiongozi wa wanajadi duniani wenye asili ya Afrika, Mwami Lukoko alisema hayo katika kusanyiko la Mwaka la wanajadi (Elombee) lililofanyika mkoani Kigoma juzi na kuhudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani na kusema kuwa na kubainisha kuwa viongozi wa taasisi lazima wawe na dhamira ya dhati ya kuwasaidia wenye mahitaji.

Kiongozi wa wanajadi duniani wenye asili ya Afrika, Mwami Lukoko katika kusanyiko la mwaka huu la Ibada ya Elombee lililofanyika Ujiji Mjini Kigoma.
Alisema kuwa mahali popote duniani viongozi na watu wenye uwezo lazima wafirikie kuwasaidia watu wenye mahitaji ili waweze kupata mahitaji yao ya msingi kuwafanya wajione sawa na wanadamu wengine ili mapungufu au hali duni waliyo nayo wasiione kama adhabu kwao ambapo katika kusanyiko hilo kiasi cha shilingi milioni moja kilikabidhiwa.
Akipokea hundi ya fedha hizo iliyotolewa kwenye kusanyiko hilo, Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Aida Nzowa ameishukuru taasisi hiyo kwa fedha hizo ambazo zitaenda kuleta tabasamu kwa wenye uhitaji wakati huu wa sikukuu ya Krismasi.

Nzowa alisema kuwa wanao idadi kubwa ya kutosha ya watu wenye uhitaji kwenye maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo hivyo kuomba watu wengi Zaidi kujitokeza kuwasaidia na kuunga mkono maneno ya Kiongozi wa Wanajadi kuwa fedha zinazoombwa kwa wahisani kwa ajili ya kuwasaidia wenye uhitaji zifike kwa walengwa.