
Tembo waua watu wanne Kenya katika kipindi cha wiki moja
Baadhi ya raia wa Kenya walilalamika siku ya Jumatano baada ya tembo waliokuwa wakiranda randa kuwaua watu wanne katika kipindi cha wiki moja kwa kile wataalamu wanaeleza mzozo kati ya binadamu na wanyamapori unaosababishwa na uhaba wa malisho.