WATUHUMIWA wawili, Marco Maginga (47) na Mwita Maginga (45), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, mkoani Mara, wakikabiliwa na shtaka la mauaji ya mwanamke Rodha Jonathani (42).
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mara zinaonyesha kwamba mauaji hayo yalitokea Oktoba 23, mwaka huu, katika Kitongoji cha Burunga, Kata ya Uwanja wa Ndege, wilayani Serengeti. Marehemu alikamatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mume wa marehemu, Mwita Charles, alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakishikiliwa na polisi kwa mahojiano, lakini hakuwa miongoni mwa waliofikishwa mahakamani leo, Desemba 23, 2025. SOMA: Baba afanya mauaji ya mtoto kisha ajinyonga
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Eligeria Rujwahuka, amebainisha kuwa kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha 196 na kifungu cha 197 cha kanuni ya adhabu, zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2023.“Mahakama imeahirisha kesi hii hadi Januari 5, 2026,” alisema Hakimu, huku watuhumiwa wakirudishwa rumande.
Nje ya mahakama, mama mzazi wa Ester Mobe ameiomba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha haki inatendeka, ili waliohusika na kifo cha mwanae wachukuliwe hatua za kisheria na iwe fundisho kwa wenye tabia za kufanya ukatili.
