Krismasi itukumbushe upendo, unyenyekevu na kusaidianaKrismasi itukumbushe upendo, unyenyekevu na kusaidiana

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka Wakristo na Watanzania wote kuitumia Sikukuu ya Krismasi kama fursa ya kuimarisha upendo, unyenyekevu na kusaidiana, ili kuendeleza mshikamano na umoja wa kitaifa.

Akitoa salamu zake za Krismasi kwa wananchi, Rais Samia amesema maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo yanapaswa kuwa kioo cha kutafakari maadili ya msingi yanayojenga jamii yenye heshima, kujaliana na kuheshimiana. Amesema Krismasi si siku ya sherehe pekee, bali ni wakati wa kuangalia wajibu wa kila Mtanzania katika kulinda na kudumisha misingi ya amani, utulivu, haki na ukweli, kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha, Rais Samia amewasihi wananchi wanaosafiri na kusherehekea na familia zao kufanya hivyo kwa amani, kuzingatia usalama na kudumisha maelewano, ili sikukuu hiyo ipite salama bila matukio yanayoweza kuhatarisha maisha au kuvuruga utulivu wa jamii. Amehitimisha kwa kuwaombea Watanzania baraka na ulinzi wa Mwenyezi Mungu, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano, upendo na umoja kama nguzo kuu ya maendeleo ya Taifa. SOMA: Papa Leo XIV kuongoza misa ya kwanza Krismasi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *