Tume ya Kupambana na Rushwa nchini Zambia (ACC) imempongeza polisi wa kike aliyekataa rushwa ya dola $50,000 kutoka kwa mshukiwa wa utakatishaji fedha katika uwanja wa ndege wa mji mkuu, Lusaka.

Sajini Ruth Nyambe, ambaye yuko kwenye Kitengo cha Viwanja vya Ndege, alikataa pesa hizo kutoka kwa mshukiwa, wakati wa taratibu za kiusalama, na inadaiwa mshukiwa huyo alipatikana akiwa na dola milioni $2.3 taslimu na vipande vinavyoaminika kuwa vya dhahabu visaba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda.

Polisi nchini Zambia wanasema tukio hilo lilifanyika Februari 5, 2025.

ACC ilisema kuwa mshukiwa huyo ambaye jina lake halikutajwa alitaka kumhonga Nyambe dola $5,000 kwanza, lakini alipokataa, mshukiwa huyo akapandisha dau hadi dola $50,000 ili aruhusiwe aendelee na safari yake na fedha hizo.

‘Uadilifu wa hali ya juu’

Kwa mara nyingine tena, Nyambe akakataa, na badala yake kuwafahamisha maafisa wa Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Zambia (DEC), na mshukiwa akakamatwa.

Mshukiwa huyo alikuwa anasafiri kutoka Lusaka hadi sehemu ambayo haikufahamika, kulingana na Lusaka Times.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *