Aidha amesema vikosi hivyo pia viliwakamata wafanyakazi 16 wa kigeni wa meli hiyo, akiongeza kuwa kukamatwa huko ni ‘pigo kubwa’ kwa biashara ya magendo. Lakini hata hivyo taarifa haikufichua uraia wa wafanyakazi hao au bendera ya meli hiyo.Iran mara kwa mara hukamata meli zinazobeba mafuta kwa madai kama hayo katika eneo hilo. Mnamo Novemba, Iran ilikamata meli nyingine ilipokuwa ikipita katika Ujia wa Bahari wa Hormuz kwa kile ilichosema ni ukiukaji, ikiwemo kubeba shehena haramu.Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakiitupia lawama Iran kwa mkururo wa mashambulizi ya meli yaliyoharibu meli za mafuta mwaka 2019, pamoja na shambulio la droni dhidi ya meli ya Israel lililosababisha vifo vya wafanyakazi wawili wa Ulaya mwaka 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *