#HABARI: Mwili wa Afisa Usafirishaji kupitia pikipiki, Hamisi Ramadhan (18) mkazi wa Kata ya Isevya Wilaya ya Tabora umekutwa umetelekezwa kwenye mtaro wa maji katika mtaa na Kata ya Malolo wilayani hapo, tukio ambalo limezua taharuki kwa kuwa pikipiki ya kijana huyo haikuonekana ambapo Jeshi la Polisi limethibitisha kuanza uchunguzi wa kina kuhusu kisa hicho.
Wakizungumza katika eneo la tukio, wamesema wameshangazwa tukio hilo ambapo walidai wameukuta mwili ukiwa na mkanda shingoni mithiri ya mtu aliyenyongwa, hali iliyowafanya watoe taarifa haraka kwenye mamlaka husika.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akidai uchunguzi wa kisayansi umeshaanza.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania