
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, ofisi ya Turk imeeleza kwamba jamii na wahamiaji walioathirika wanapaswa kupata msaada wote muhimu ili kurejea nyumbani salama.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi takriban watu 47 wameuawa huku zaidi ya milioni moja wakihamishwa katika kipindi cha wiki tatu za mapigano ya mpakani yaliyohusisha mizinga, vifaru, droni na ndege za kivita.
Makubaliano yaliyofikiwa yamezitaka pande zote kuheshimu mikataba ya kupiga marufuku mabomu ya ardhini, kuepuka kusambaza habari za uongo, kuendelea na mipango ya kuweka mipaka, na kushirikiana kupambana na uhalifu wa kimataifa—hasa ulaghai wa mtandaoni unaoendeshwa na magenge ya uhalifu nchini Cambodia.