WAKATI timu za Taifa zikiendelea na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayopigwa kule Morocco, kocha mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves ameshindwa kuvumilia kwa kusema anafurahishwa na kiwango cha mastaa wa kikosi hicho wanaoshiriki michuano hiyo.

Pedro amesema amekuwa akiifuatilia michuano hiyo inayoshiriki timu za nchi 24 ikiwamo Tanzania inayoshiriki mara ya nne tangu mwaka 1980 na amekuwa akivutiwa na wachezaji wa klabu hiyo wanayoiwakilisha nchi zao za taifa.

Yanga katika michuano hiyo ina wachezaji sita wakiwamo wanne wa timu ya taifa, Taifa Stars ambao ni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Offen Chikola, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakar Mwamnyeto wakati Diarra Djigui akiwa na Mali na Prince Dube Zimbabwe.

Akizungumza na Mwanaspoti, Pedro aliyeiwezesha Angola kufuzu fainali hizo wakati akiinoa kabla ya kuajiriwa Yanga, amesema kwa upande anaona michuano hiyo ikiwaongezea kitu kikubwa mastaa hao kwani wamekuwa na kiwango bora zaidi katika kila mechi wanazocheza.

MASTA 01

Amesema jambo pekee analoomba ni  wachezaji walipo AFCON wasirejee na majeraha kutokana na Yanga kuwa na kibarua kizito cha mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na ile ya Ligi Kuu Bara zitakazorejea baada ya fainali hizo za Morocco.

Yanga iliyopo Kundi B katika Ligi ya Mabingwa ikishika nafasi ya pili kwa sasa ina mechi mbili mfululizo dhidi ya Al Ahly ya Misri zitakazochezwa kati ya Januari 23 na 30 kabla ya kumalizana na AS FAR.

 kisha itacheza na JS Kabylie ya Algeria baada Februari mwakani.

MASTA 02

“Mechi hizi zina faida kubwa sana hasa kwa upande wa utimamu wa miwili, wachezaji wanakuwa sawa muda wote kutokana na mazoezi wanayopewa na ile akili ya mashindano ambayo wanakuwa nayo wakati wote.

“Hii ni fursa kubwa kwa sababu muda sio mrefu tutakuwa na michuano ya CAF mbele yetu kwa hiyo kama wakirejea bila majeraha basi kikosi kitakuwa na wachezaji waliobora sana.

Pedro amesema, wapo wachezaji ambao wameendela kuonyesha kiwango bora katika mechi walizocheza, mfano mzuri ni Diarra na wengine.

MASTA 03

“Nafurahishwa sana na viwango vya wachezaji walioko kwenye michuano ya Afcon, licha ya kwamba kuna wachezaji kutoka timu zingine ila bado wameweza kupata nafasi na wanaitendea haki.

“Nikianza na kipa wa Mali, Djigui Diarra, Prince Dube na wale wa Taifa Stars wote wananifanya nifurahie kila mechi wanayocheza kutokana na ubora waliouendeleza hadi sasa katika AFCON.”

Wakati michuano hiyo ikiendelea Pedro na mastaa waliosalia ndani ya kikosi hicho wanaendelea kujinoa kabla ya kuanza kuwasha moto katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026 ikiwa Kundi C sambamba na KVZ na TRA United.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *