Nchini Guinea, matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, uliofanyika Jumapili, yanatarajiwa kutangazwa leo, huku kiongozi wa kijeshi Mamady Doumbouya, akitarajiwa kutangazwa mshindi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Doumbouya mwenye umri wa miaka 41, unatarajiwa kuhalalisha uongozi wake, na kutuma ujumbe kwa jumuiya ya Kimataifa kuwa, amefanikiwa kurejesha nchi hiyo kwenye utawala wa kidemokrasia.

Wagombea wakuu wa upinzani, wakiongozwa na Cellou Dalein walizuiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo wa Jumapili iliyopita, na kuwataka wafuasi wake kutoshiriki, wakiutaja uchaguzi huo kama kichekesho.

Hata hivyo, Doumbouya, anapambana na wagombea wengine nane, wanaoelezwa ni dhaifu, wakiwemo Abdoulaye Yéro Baldé na  Faya Millimouno.

Uchaguzi huu umekuja, miaka minne baada ya Doumbouya, kuongoza mapinduzi ya kijeshi na kuchukua madaraka kutoka kwa aliyekuwa rais Alpha Conde.

Wakati matokeo ya mwisho, yakitarajiwa siku ya Jumanne au Jumatano, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Djenabou Toure, ametangaza kuwa zoezi la kuhesabu na kujumuisha kura linaendelea vema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *