
Rais Zelensky amesema hayo siku moja baada ya mazungumzo na Rais Donald Trump ya kuvimaliza vita na Urusi nchini mwake yaliyofanyika Florida, Jumapili.
Amewaambia waandishi wa habari kwamba, alimweleza Trump kwamba tayari wamekuwa vitani kwa karibu miaka 15 na kumsisitizia wanahitaji dhamana hiyo iwe ya muda mrefu zaidi cha hadi miaka 50, na kwamba Trump ameahidi kulizingatia hilo.
Trump mapema, alisema Ukraine na Urusi wanakaribia kufikia makubaliano ya amani, ingawa alikiri kwamba mazungumzo hayo ni magumu na bado yanaweza kuvunjika.