
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, atakutana na rais Donald Trump huko Florida saa chache zijazo, wakati huu Marekani ikiendelea kushinikiza utekelezwaji kikamifu kwa mkataba, uliomaliza vita kwenye ukanda wa Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati wa mazungumzo hayo, Netanyahu anarajiwa pia kuleta suala la namna Israeli na Marekani, zinavyoweza kuendelea kushirikiana, kutekeleza mashambulio zaidi dhidi ya Iran.
Huu ni mkutano wa tano kati ya viongozi hao wawili, kufanyika nchini Marekani, wakati huu maafisa wa Marekani wakohofia kuwa mkataba wa kusitisha vita kwenye ukanda wa Gaza, unatekelezwa kwa mwendo wa kinyonga kati ya Israel na Hamas.
Kuelekea utelezwaji wa awamu ya pili wa mkataba huo, Trump alisema Netanyahu, aliomba kikao hicho, ili wakati huu kukiwa na mpango wa kutangazwa kwa serikali ya kuongoza Gaza na uwepo kwa kikosi cha Kimataifa katika eneo hilo.
Msemaji wa serikali ya Israeli Shosh Bedrosian, amesema Netanyahu atazungumza kuhusu utekelezwaji wa awamu ya pili ya mkataba huo, unaolenga kuwapokonya silaha, Hamas na kuhakikisha kuwa Gaza inasalia bila makundi yenye silaha.