Kauli za rais zilijiri baada ya viongozi hao kukutana kwa mazungumzo kufuatia kile Trump alisema ni mazungumzo “mazuri zaidi” ya saa mbili na nusu kwa simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye uvamizi wake dhidi ya Ukraine ulianzisha vita karibu miaka minne iliyopita. Trump alisisitiza kwamba anaamini Putin bado anataka amani, hata kama Urusiilianzisha mashambulizi mengine dhidi ya Ukraine wakati Zelenskyy akisafiri hadi Marekani kwa ajili ya duru ya karibuni ya mazungumzo.

Trump na Zelenskyy walikiri kwamba bado kuna masuala magumu, ikiwa ni pamoja na kama Urusi inaweza kumiliki eneo la Ukraine inalolidhibiti, pamoja na dhamana ya usalama kwa Ukraine ili kuhakikisha kuwa haivamiwi tena katika siku zijazo. Baada ya majadiliano yao, waliwapigia simu kundi kubwa la viongozi wa Ulaya, akiwemo Ursula von der Leyen, rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, na viongozi wa Finland, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Poland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *