Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron metangaza leo Jumatatu, Desemba 29, mkutano wa washirika wa Kyiv huko Paris mapema mwezi Januari kujadili dhamana za usalama kwa Ukraine ndani ya mfumo wa makubaliano ya amani na Urusi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Tutazileta pamoja nchi za muungano wa wanaojitolea huko Paris mapema mwezi Januari ili kukamilisha michango halisi ya kila nchi,” ameandika Emmanuel Macron, ambaye hapo awali alizungumza na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Marekani Donald Trump, pamoja na viongozi wengine kadhaa wa Ulaya

“Tunapiga hatua katika dhamana za usalama ambazo zitakuwa muhimu katika kujenga amani ya haki na ya kudumu,” amesema kiongozi huyo wa Ufaransa, ambaye pia amezungumza na Volodymyr Zelensky. 

Tangazo hili linakuja wakati Volodymyr Zelensky na Donald Trump walipokutana mnamo Desemba 28 katika makazi ya rais wa Marekani huko Florida, huku rais Donald Trump akionekana kuwa na matumaini makubwa, ingawa pia anakwepa, kuhusu utatuzi wa haraka wa mzozo ambao umeendelea tangu mwezi Februari 2022.

Ukraine na Marekani bado hazijafikia mwafaka juu ya masuala mawili makuu: udhibiti wa maeneo ya ardhi na udhibiti wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia — lakini hapo awali Zelensky alisema anatumai kuyajadili yote mawili na Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *