
Utata unaongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuhusu madai ya uvumilivu wa serikali kwa matamshi ya chuki dhidi ya Watutsi. Rais Félix Tshisekedi alikutana mnamo Desemba 22 na Wakongo wawili kutoka Marekani, Jean-Claude Mubenga na Kalonji Kabamba wa Mulumba. Maafisa wanasema mazungumzo hayo yalilenga umoja wa kitaifa na uhuru. Lakini wakosoaji wanasema mkutano huo ulituma ujumbe usio sahihi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku iliyofuata, Mubenga alichapisha maudhui ya uchochezi mtandaoni, akitumia lugha ya kudhalilisha utu na kusifu makundi yenye silaha yanayoshutumiwa kuwalenga raia wanaozungumza Kinyarwanda.
Wakati huo huo msemaji wa jeshi Meja Jenerali Sylvain Ekenge amesimamishwa kazi kufuatia matamshi yenye utata kuhusu wanawake wa Kitusi.
Jeshi linasema matamshi hayo yalikuwa ya kibaguzi na hayaonyeshi msimamo wa serikali, jeshi, au Rais Félix Tshisekedi, akisisitiza kwamba yalitolewa kwa njia ya kibinafsi.
Watutsi ni kundi la kikabila linaloishi kote Rwanda na mashariki mwa Kongo, na uwepo wao unahusishwa kwa karibu na miongo kadhaa ya migogoro na uhusiano mbaya kati ya DRC na Rwanda.
Soma piaDRC: Sylvain Ekenge msemaji wa FARDC amesimamishwa kazi