Chini Côte d’Ivoire chama tawala cha RHDP kimeimarisha wingi wake kamili katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya Jumamosi, Desemba 27. Chama cha Rais Alassane Ouattara, kilichochaguliwa tena miezi miwili iliyopita kwa karibu 90% ya kura, kimeshinda karibu 77% ya viti, kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Abidjan, Bineta Diagne

Chama cha RHDP kimefanya vizuri katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita: kimepata viti 197, sawa na 34 zaidi ya mwaka 2021. Chama kimeimarisha umiliki wake katika ngome zake, haswa katika mikoa ya kaskazini. Kilipata ushindi mnono huko Boundiali na Odienné, ambapo kilipata 100% ya kura. Cama cha RHDP kimepata 99.92% ya kura huko Korhogo na 98.95% huko Bouaké (eneo la kati). RHDP pia ilithibitisha nafasi yake imara katika eneo la Haut-Sassandra.

Kwa chaguzi hizi, RHDP iliwasilisha idadi kubwa zaidi ya wagombea. Miongoni mwao walikuwa maafisa wengi wa chama na mawaziri ambao pia walipata matokeo mazuri katika majimbo yao: 99.93% kwa Makamu wa Rais huko Tafiré, 88% ya kura kwa Waziri wa Ulinzi wa sasa huko Abobo, na 100% kwa Waziri wa Mawasiliano huko Koni.

Pia ni muhimu kuzingatia kwamba RHDP imefanya vizuri kusini mwa nchi, na pia katika maeneo ambayo yamekuwa yakipinga chama hiki. Hivi ndivyo ilivyokuwa huko Abengourou, mashariki, ambapo RHDP ilishikilia moja ya viti sita mwaka wa 2021. Wakati huu, ilishinda viti vyote sita.

Kushuka pakubwa kwa PDCI

Uchunguzi mwingine kutoka kwa uchaguzi huu: kupungua kwa kasi kwa Chama cha PDCI, chama kinachoongozwa na Tidjane Thiam. PDCI ilishinda viti 32: nusu ya idadi ya viti vilivyopatikana mwaka 2021. Ingawa PDCI ilishikilia nafasi yake katika ngome yake ya Daoukro, ilishindwa kupata ushindi muhimu: Yamoussoukro, ambapo inashikilia umeya, ilishindwa kwa tiketi ya RHDP ya Augustin Thiam – kaka yake Tidjane Thiam – na Souleymane Diarrassouba, Waziri wa Biashara.

Huko Abidjan, PDCI imedumisha uwepo wake katika wilaya za Cocody, Plateau, na Port-Bouët. Hata hivyo, chama hicho kimepata vikwazo vingi, kama inavyothibitishwa na kushindwa kwa Alphonse Djédjé Mady huko Haut-Sassandra. Pia kimeshindwa katika wilaya ya Marcory, Jacqueville, Abengourou, na Yopougon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *