Katika juhudi za kuendelea kukuza zao la kahawa nchini, Bodi ya Kahawa imegawa zaidi ya miche 5,000,000 kwa wakulima wa zao hilo mikoa ya Nyanda za juu Kusini wakilenga wakulima kupata miche bora, kuongeza uzalishaji na kuimarisha uchumi kwa wakulima na kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa taifa.
Meneja wa Kanda ya Mbeya, Ezekia Mwakyoma amesema wameamua kutoa miche hiyo bure kipaumbele kikielekezwa zaidi kwa vijana na wanawake, kutokana na kutambua mchango na nguvu kubwa waliyonayo katika sekta ya uzalishaji wa zao hilo.
#AzamTVUpdates
✍ Joyce Lyanda
Mhariri | @claud_jm