#HABARI: Uongozi wa Manispaa ya Kibaha mkoani Pwani umesimamisha uzalishaji katika kiwanda cha Fortune Paper kufuatia malalamiko kutoka kwa wakazi wa Kata ya Misugusugu.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya maji yanayotoka kiwandani humo kuingia kwenye makazi na mashamba ya wananchi, hali inayosababisha uharibifu wa mazao na kuhatarisha afya za jamii.
Wakazi hao wameeleza kuwa kero hiyo imekuwa ikiwaumiza kwa muda mrefu, jambo lililopelekea uongozi kuchukua hatua hiyo ya dharura kusitisha uzalishaji.
Kusitishwa kwa shughuli za kiwanda hicho kunalenga kutoa nafasi ya kutatua changamoto hiyo ya mazingira ili kulinda usalama na mali za wananchi wa maeneo jirani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.