#HABARI: Mfuko wa Bodi ya Barabara mkoani Mtwara umetoa muda wa siku 14 kwa Mkandarasi Mshauri kuhakikisha barabara za michepuko zinapitika bila kero. Agizo hili limetolewa ili kupisha ujenzi wa barabara ya uchumi kutoka Mtwara – Newala hadi Masasi, yenye urefu wa kilomita 160, inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Lengo la agizo hilo ni kuhakikisha kuwa barabara hizo za michepuko za muda haziwi kero kwa watumiaji wa vyombo vya moto na abiria wakati ujenzi ukiendelea. Baadhi ya madereva na wakazi wa Kata ya Mtibwilimbwi wameeleza kero wanazopata kutokana na hali ya sasa ya barabara hizo, wakisisitiza umuhimu wa kufanyiwa marekebisho ya haraka.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.