Kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki duniani Papa Leo wa XIV, anakutana Vatican, kwa siku mbili kuanzia leo Jumatano hadi Alkhamisi na makadinali kutoka duniani, baada ya kuweko miito ya kutaka  kanisa hilo lizingatie mfumo wa uongozi wa ushirikishaji katika utoaji maamuzi.

Papa Leo alaani waziwazi hali ya Wapalestina huko Gaza

Mkutano huo unaofahamika kama baraza maalum la makadinali, ni wa kwanza kwa papa Leo  tangu alipochaguliwa kuliongoza kanisa hilo Mei mwaka jana baada ya kifo cha mtangulizi wake Papa Francis.

Vyanzo vya kanisa hilo mjini Vatican  vimesema kwamba makadinali wanataka kuwa na dhima kubwa zaidi katika usimamizi wa kanisa kwenye ngazi ya kimataifa.  Kanisa Katoliki

Mkutano huo pia huenda ukatowa mwelekeo kuhusu namna uongozi wa Papa Leo utakavyokuwa na mipango yake kwa kanisa hilo duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *