
Rais wa Marekani Donald Trump amezindua shambulio jipya dhidi ya diplomasia ya hali ya hewa, akiamuru Marekani ijiondoe kutoka kwa mkataba na kamati ya kisayansi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, miongoni mwa mashirika kadhaa yaliyotambuliwa kuwa hayatumiki tena kwa “maslahi ya Marekani”, White House imetangaza.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Agizo la kiutendaji lililoosainiwa na rais wa Marekani linaagiza Marekani ikujiondoa kutoka kwa jumla ya mashirika 66, karibu nusu yake ambayo yana uhusiano na Umoja wa Mataifa, Ikulu ya White House imeongeza.
Miongoni mwa hayo ni Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC), mkataba wa msingi wa mikataba mingine yote ya kimataifa ya hali ya hewa, uliohitimishwa mwaka wa 1992 katika Mkutano wa Rio Earth. Ilikuwa ndani ya mfumo wa UNFCCC ambapo Mkataba wa Paris wa 2015 ulisainiwa baadaye, ambapo Donald Trump alijiondoa kwa mara ya pili aliporudi Ikulu ya White House mwaka mmoja uliopita. Wakati wa muhula wake wa kwanza, pia alijiondoa kutoka kwa Mkataba wa Paris, lakini si kutoka kwa UNFCCC, na kuruhusu Marekani kuendelea kushiriki katika mikutano ya kila mwaka ya hali ya hewa.
Hatua hii mpya ya kujiondoa ni “ishara nyingine kwamba utawala huu wa kimabavu na unaopinga sayansi umeazimia kutoa kafara ustawi wa raia na kuvuruga ushirikiano wa kimataifa,” Rachel Cleetus wa shirika la Union of Concerned Scientists ameliambia shirika la habari la AFP.
Mashirika yanayohusiana na hali ya hewa yamelengwa hasa
Agizo hilo la utendaji pia linagiza kujiondoa kwa Marekani kutoka kwa Jopo la wataalamu wa masuala ya kisayansi la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (IPCC), mamlaka inayoongoza katika sayansi ya hali ya hewa, pamoja na mashirika mengine yanayohusika katika kulinda sayari, kama vile Shirika la Kimataifa la Nishati Mbadala (IRAC), Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), na UN-Water.
Mnamo mwezi Septemba, akizungumza kutoka jukwaa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Donald Trump alichochea athari kali kwa kuanzisha shambulio la moja kwa moja dhidi ya sayansi ya hali ya hewa, akiita ongezeko la joto duniani “udanganyifu mkubwa zaidi katika historia yetu” na kusifu makaa ya mawe kama “safi na nzuri.”
Wakati utawala wa Trump pia ukishambulia mara kwa mara Malengo ya Maendeleo Endelevu yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuboresha mustakabali wa ubinadamu, kama vile kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kukuza usawa wa kijinsia, agizo la kiutendaji lililochapishwa siku ya Jumatano pia linaamuru kujiondoa kwa Marekani kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA). Washington ilikuwa tayari imetangaza miezi kadhaa iliyopita kwamba itapunguza ufadhili kwa shirika hili linalobobea katika afya ya mama na mtoto.
Pia linalolengwa ni Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), ambalo mkuu wake, Rebeca Grynspan, ni mgombea anayetarajia kumrithi António Guterres kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Kujiondoa huku kunakuja juu ya yale yaliyotokana na Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi na UNESCO (Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa), ambalo Marekani ilikuwa imejiunga nalo chini ya utawala wa Joe Biden. Donald Trump pia ameiondoa Marekani kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).