Hadi sasa, mashabiki hawajaridhishwa na kiwango cha Morocco, licha ya ushindi wa 2–0 dhidi ya Comoros na sare ya 1–1 na Mali ambapo  walizomewa na mashabiki. Kwa mara nyengine tena nahodha Achraf Hakimi amewataka mashabiki kuwaunga mkono, akisema umoja wao unaweza kuifanya Morocco kuwa mabingwa wa AFCON.

Kocha Regragui anasisitiza kuwa ushindi ndio jambo la msingi kuliko uchezaji wa kuvutia, akiamini uzoefu wa kikosi chake utawasaidia kubeba taji ambalo Morocco haijashinda kwa zaidi ya miaka 50.

Kwa upande wao, Cameroon wanaingia kwenye mchezo huo bila shinikizo kubwa. Mabingwa mara tano wa Afrika, tayari wamevuka matarajio kwa kufika robo fainali baada ya rais wa shirikisho la soka Samuel Eto’o, kumfuta kazi kocha Marc Brys na kumteua kocha mzawa, David Pagou.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *