
Kwa mujibu wa taarifa jana ya Ikulu ya Tanzania, Patrobas Katambi, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya George Simbachawene ambaye ametenguliwa. Kabla ya uteuzi huo, Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.Rais Samia pia amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum).Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Aidha nafasi ya Kabudi imechukuliwa na Paul Makonda ambae awali alikuwa naibu wake.