Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri Januari 8.

Mabadiliko hayo ambayo yamefanyika ndani ya siku 54 tangu kutangazwa kwa Baraza la Kwanza la Mawaziri la kipindi cha pili cha serikali ya Awamu ya Sita.

Paul Christian Makonda, ambae awali alikuwa Naibu Waziri wa Habari, hivi sasa amepewa Wizara kamili ya Habari, Sanaa na Utamaduni, akichukua nafasi ya Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi, ambae sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum).

Rais Samia pia, alitengua uteuzi wa Boniface George Simbachawene ambae alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na nafasi yake kuchukuliwa na Patrobas Paschal Katambi, ambae awali alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Makonda na Katambi ni miongoni mwa mawaziri waliopanda kwa kasi ndani ya muda mfupi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *