Mwanasiassa huyo wa kihafidhina anapanga kukutana na mwenzake wa Marekani Marco Rubio kwa ajili ya mazungumzo Jumatatu ijayo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje amesema Ijumaa.

Amesema ajenda kuu kwenye mazungumzo hayo yatajikita kwenye ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili, msaada zaidi kwa Ukraine ushirikiano wa kanda ya India-Pasifiki pamoja na sera za kiusalama.

Kulingana na msemaji huyo, Wadephul anatarajiwa kuweka kituo Iceland katika safari yake hiyo ya kuelekea Marekani ambako atakutana na mwenzake Katrín Gunnarsdóttir. Wadephul tayari alikuwa amekutana na Gunnarsdóttir mjini Berlin mwanzoni mwa Desemba.

Kitisho cha Trump kuichukua Greenland chazidi kuibua hofu

Msemaji huyo hata hivyo hakutangaza ikiwa waziri Wadephul atasimama pia huko Greenland. Amesema safari hiyo ilikuwa ni ishara kubwa ya uhusiano wa karibu wa pande hizo mbili, lakini pia umuhimu wake kwa washirika wa NATO wa Ulaya.

Denmark Copenhagen 2026 | Bendera ya Greenland katika Jumba la Tivoli wakati kukishuhudiwa mvutano na Marekani
Bendera ya Greenland katika Jumba la Tivoli wakati kukishuhudiwa mvutano na Marekani inayotaka kuluchukua eneo hiloPicha: Ida Marie Odgaard/Ritzau Scanpix/AFP

Rais wa Marekani Donald Trump ameonyesha nia inayozidi kuongezeka ya kulichukua eneo la Greenland, ambalo ni sehemu ya mshirika wa NATO, Denmark.

Katika mahojiano na New York Times yaliyochapishwa Alhamisi, Trump alieleza kwa mara nyingine juu ya maslahi yake kwa Greenland kuanzia ya usalama wa taifa wa Marekani hadi maliasili zinazopatikana kwenye kisiwa hicho.

Kuichukua Greenland kwa nguvu kunamaanisha kumshambulia mwanachama mwenzake wa NATO. Na alipoulizwa ni kipaumbele gani cha juu zaidi, ama kuipata Greenland au kudumisha ushirikiano wa NATO, Trump hakutaka kujibu moja kwa moja, lakini alikiri kwamba “huenda kukawa na chaguo.”

Bendera ya Umoja wa Mataifa
Berlin imeeleza kusikitishwa na hatua ya Marekani ya kujiondoa kwenye mashirika ya kimataifaPicha: Michael Nguyen/NurPhoto/picture alliance

Berlin yafadhaishwa na Marekani kujiondoa mashirika ya kimataifa.

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje alielezea masikitiko yake baada ya Marekani kutangaza kujiondoa kwenye mashirika 66 ya kimataifa katika maeneo kama vile mazingira na hali ya hewa, usawa wa kijinsia, elimu, pamoja na kukuza demokrasia, asasi za kiraia na utawala wa sheria.

Alisema changamoto za kimataifa kama vile vita, njaa na uharibifu wa mazingira zinaweza kushughulikiwa kwa ushirika wa kidunia. Berlin itaendelea kuzungumza na Washington “ili kuwa na uelewa wa pamoja wa jinsi ushirikiano wa kimataifa na maslahi yao ya pamoja unavyoweza kuendelezwa zaidi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *