Msemaji wa bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf, ameliambia shirika la habari la Al Araby kwamba shambulizi lolote la Marekani litapelekea mashambulizi makubwa dhidi ya kambi za kijeshi za mataifa hayo mawili.

Awali rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwaunga mkono waandamanaji walioingia mitaani. Alitangaza kuwa huenda akatumia nguvu za kijeshi kuishambulia nchi hiyo iwapo waandamanaji watauliwa.

“Iran ipo kwenye matatizo makubwa. Naona kwamba watu wanaendelea kuandamana katika miji mingi, hatua ambayo hakuna mtu aliyefikiria ingewezekana wiki chache zilizopita. Tunaangalia hali hiyo kwa makini sana. Nimetoa kauli kali kwamba wakianza kuwaua watu kama walivyofanya hapo awali, tutajihusisha. Tutawalenga pale panapoumiza.”

Kulingana na shirika la kutetea haki za binaadamu lililo na makao yake Marekani (HRANA), idadi ya waliouwawa kufuatia maandamano yaliyodumu kwa wiki 2 sasa, imepanda na kufikia 116 huku zaidi ya 2,600 wamekamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *