
Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumapili, Januari 11, kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez, ambaye aliteuliwa madarakani baada ya Marekani kumkamata Nicolas Maduro.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Alipoulizwa kama alipanga kukutana naye, Trump aliwaambia waandishi wa habari, “Wakati fulani, nitafanya hivyo,” akiongeza ndani ya ndege ya Air Force One kwamba Washington ilikuwa ikifanya kazi “vizuri sana” na Caracas.
Wakati huo huo raia wa Venezuela wameendelea kusubiri kuachiwa huru idadi kubwa ya wafungwa wa kisiasa kufuatia ahadi iliyotolewa na rais wa mpito Delcy Rodriguez Alhamisi wiki iliyopita.
Serikali ya rais wa mpito Delcy Rodriguez Alhamisi iliyopita ilianza kuwaachilia wafungwa waliofungwa chini ya Maduro katika ishara ya uwazi, baada ya kuahidi kushirikiana na Marekani kuhusu madai yake ya mafuta ya Venezuela.
Serikali ilisema idadi kubwa ya wafungwa itaachiliwa lakini makundi ya haki za binadamu na upinzani yanasema ni takriban 20 tu wameachiliwa huru tangu wakati huo, wakiwemo viongozi kadhaa mashuhuri wa upinzani.
Naye kiongozi aliyeondolewa madarakani Nicolas Maduro amedai kwa ukaidi kutoka kwenye chumba chake cha mahabusu katika gereza la Marekani kwamba anaendelea vizuri baada ya kukamatwa na vikosi vya Marekani wiki moja iliyopita.