
Ripoti ya kutetea haki za binadamu ya Human Rights Watch, imesema vitendo vya unyanyasaji wa kimapenzi, vinatumiwa kama silaha ya vita, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Human Rights Watch inasema, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia idadi ya watu, visa zaidi ya 80,000 vya ubakaji, viliripotiwa katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kusini, kati ya Januari hadi Septemba mwaka 2025.
Takwimu hizi zinaonesha ongezeko la visa hivyo vya ubakaji kwa asilimia 30-ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2024.
Kwa mujibu wa wale waliohojiwa, wanawake na wasishana waliodhulumiwa, waliotekeleza visa hivyo ikiwa ni pamoja na ubakaji ni pamoja na wapiganaji wa Wazalendo, wanaoshirikiana na wanajeshi wa serikali FARDC, waasi wa M23/AFC, waasi wa CODECO na ADF.
Mbali na makundi ya waasi, baadhi ya wanawake walinyanyanswa na wanajeshi kwa mujibu wa Human Rights Watch, huku wengine wakibakwa mashambani na maeneo yao ya kazi.
Licha ya kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya wahusika, Human Rights Watch inaonya kuwa tangu kurejea kwa waasi wa M23, visa vya unyanyasaji vimeongezeka na inahofia ni vipi walioathiriwa watashughulikiwa baada ya Marekani kupunguza misaada hasa ya kifedha.