
Serikali ya Afrika Kusini imewatahadharisha wananchi wake katika mkoa wa Limpopo kuwa waangalifu baada ya wanyama hatari ikiwemo mamba na viboko, kuonekana katika makazi ya watu kufuatia mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika mabwawa na mito.
Huduma ya Hali ya Hewa ya Afrika Kusini (SAWS) siku ya Jumanne imetoa tahadhari ya Kiwango cha 9 na 6 inayotahadharisha kuhusu hali mbaya ya hewa kwa mikoa ya Limpopo, Mpumalanga na Gauteng, ikiwatahadharisha watu dhidi ya mafuriko, barabara kufungwa, maporomoko ya udongo na mawe, huku mvua kubwa zikiendelea.
Mamlaka za mikoa zimesema mamba wameonekana katika makazi ya watu maeneo ya Makuleke na Mhinga, nje ya Malamulele. Mamba wanaaminika kutoka katika mito ya karibu na mabwawa yaliyojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Taifa SABC.
Maafisa wa mazingira nao wametahadharisha kwamba baadhi ya wanyama wengine wa mwituni, ikiwemo viboko, wanaweza kuonekana baada ya maji kuongezeka, na kuwataka wananchi kuepuka maeneo yenye mafuriko, na kutoa taarifa haraka iwapo watawaona wanyama hao.
Jitihada za uokozi
