Merz: Dalili za mwisho za utawala wa Iran zinaonekanaMerz: Dalili za mwisho za utawala wa Iran zinaonekana

Akiwa ziarani nchini India, Merz amesema wakati serikali inapolazimika kutumia nguvu ili kubaki madarakani, mara nyingi huwa ni ishara kwamba utawala huo unafikia ukingoni.

Amelaani vikali hatua ya vikosi vya usalama vya Iran kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, akizitaja kuwa “hazina uwiano na ni za kikatili.”

“Ninatoa wito kwa uongozi wa Iran kuwalinda wananchi wake badala ya kuwatisha. Tunalaani vikali matumizi ya nguvu ambayo uongozi wa Tehran unatumia dhidi ya watu wake. Vurugu hizi sio ishara ya nguvu, bali ni ishara ya udhaifu. Vurugu hizi lazima zikome.”

Iran imekumbwa na maandamano makubwa tangu Disemba 28. Kilichoanza kama malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu kushuka kwa thamani ya riale na hali ngumu ya kiuchumi, kimegeuka na kuwa maandamano ya kitaifa dhidi ya utawala wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake Oslo, Iran Human Rights, takriban watu 648 wameuawa tangu maandamano hayo yalipoanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *