
Ukandaizaji dhidi ya harakati za maandamano zinazoendelea nchini Iran umesababisha idadi iliyothibitishwa ya vifo vya watu 2,571, wakiwemo waandamanaji 2,403 na watu 147 wanaohusishwa na serikali, shirika la haki za binadamu la HRANA lenye makao yake nchini Marekani limeripoti leo Jumatano.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shirika hilo limebainisha kuwa watoto 12 na raia tisa ambao hawakuwa waandamanaji pia ni miongoni mwa waathiriwa.
Hukumu ya kifo ya mmoja wa waandamanaji kutekelezwa leo leo
Katika ujumbe uliorushwa siku ya Jumanne kwenye mtandao wa kijamii wa X kwa Kifarsi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema kwamba mamlaka ya Iran inapanga kumuua Erfan Soltani leo Jumatano, ikibainisha kuwa “zaidi ya Wairan 10,600 wamekamatwa na utawala wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kudai haki zao za msingi. Erfan Soltani, 26, aliyehukumiwa kifo Januari 14, ni miongoni mwao.” Erfan Soltani hajapewa wakili au kesi nyingine baada ya hukumu yake ya kifo, kulingana na mmoaj wa ndugu zake ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama.
Je, harakati hii ya maandamano inatofautianaje na maandamano ya awali ya kiraia?
Ikilinganishwa na harakati za maandamano za miaka kumi iliyopita, ambazo kulishuhudiwa maandamano dhidi ya gharama kubwa ya maisha na kupanda kwa bei ya petroli, na kufuatia kifo cha Mahsa Amini, aliyekamatwa kwa kukukiuka uvaaji hijabu, wakati huu kunashuhudiwa mabadiliko na msimamo mkali wa maandamano hayo. Yamekuwa maandamano yenye kaulimbiu za kisiasa sana zinazounga mkono ufalme wa zamani na kurudi kwa familia ya Pahlavi, pamoja na kaulimbiu kali dhidi ya serikali.
Pia kunashuhudiwa maandamano makubwa sana katika miji midogo ya majimbo ambayo Wairan wengi hawaijui. Hii ni miji ambayo majina yake hayajawahi kusikika. Hiii miji midogo au miji yenye idadi ya wafanyakazi maskini sana ambapo raia wake wameingia mitaani.
Siku ya Jumanne, Januari 13, Donald Trump aliwahimiza waandamanaji wa Iran kuendelea na harakati zao hadi watakapopindua mamlaka, akiahidi kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba “misaada iko njiani,” bila kutoa maelezo zaidi. Aliahidi jibu “kali sana” ikiwa waandamanaji waliokamatwa watauawa.
