Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba, ameagiza watendaji wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi cha Kikanda – Mwanza kuhakikisha kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi mkubwa.

Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza chneye thamani ya Sh19.8 bilioni.

“Hii ni kazi ya kuokoa maisha. Uzembe, kusinzia au kuchelewesha kutoa msaada ni kuhatarisha maisha ya Watanzania. Kituo hiki lazima kifanye kazi kwa saa 24.”

Dkt Mwigulu amesema ujenzi wa kituo hicho ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kuwatumikia Watanzania na kujali changamoto zao.

“Kituo hiki kilikuwa kijengwe mwaka 2018 lakini kilisimama baada ya wenzetu kujitoa. Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan akasema tutakijengai kwa fedha zetu ili wavuvi waweze kupata huduma ya usalama katika kazi zao”

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *