Libya imetangaza siku ya Jumamosi kwamba imesaini mkataba wa miaka 25 wa mafuta wa dola bilioni 20 na kampuni ya nishati ya Ufaransa TotalEnergies na kampuni ya nishati ya Marekani ConocoPhillips.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abdelhamid Dbeibah alibaini kwamba mkataba huo ungezalisha mapato ya zaidi ya dola bilioni 370 katika mkataba wa miaka 25, na kuongeza kwamba ulifadhiliwa kikamilifu nje ya bajeti ya serikali.

Tangazo hilo lilikuja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nishati na Uchumi wa Libya huko Tripoli, uliohudhuriwa na mshauri wa Rais wa Marekani Donald Trump kwa Mashariki ya Kati, Massad Boulos, pamoja na maafisa wengine, wakiwemo wale kutoka Uturuki na Misri.

Massad Boulos aliuelezea mkutano huo wa nishati kama “fursa ya kuwa mshirika mkuu wa kiuchumi wa Marekani.” Aliongeza kuwa tukio hilo ni “tukio linalowezekana la uzinduzi wa Libya kama taifa kubwa la nishati duniani.”

Abdelhamid Dbeibah alibainisha kwamba Libya pia ilikuwa ikijiandaa kusaini makubaliano na kampuni kubwa ya Marekani ya Chevron kwa ajili ya utafutaji na maendeleo ya uzalishaji, pamoja na makubaliano tofauti na Misri ili kusaidia huduma katika sekta hiyo.

Mwaka wa 2025 ulikuwa mwaka ambao ilionekana wazi kwamba makampuni mengi makubwa, lakini pia makampuni madogo, yanataka kuingia katika soko la Libya. Na pia kuna yale yanaotaka kuongeza uwepo wao. Hivi ndivyo ilivyo kwa Eni, TotalEnergies, na ConocoPhillips. Pia kampuni ya Exxon inajipanga kurudi…

Zabuni mpya

Serikali mbili kwa sasa zinawania madaraka nchini Libya: Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA) iliyoko Tripoli, ikiongozwa na Abdelhamid Dbeibah na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, na nyingine huko Benghazi (mashariki), ikiongozwa na Marshal Khalifa Haftar na wanawe.

Masoud Suleman, Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Mafuta, alibaini kwamba zabuni mpya ya utafutaji wa mafuta na gesi itatangazwa mwezi ujao. Zabuni ya mwisho ya utafutaji wa hidrokaboni nchini Libya, mwaka 2007-2008, ililenga utafutaji wa gesi asilia. Mamlaka imejaribu kuvutia makampuni makubwa ya nishati duniani kurudi nchini humo baada ya miaka mingi ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa na viwango vya uzalishaji vinavyobadilika.

Kwa sasa Libya inazalisha takriban mapipa milioni 1.5 kwa siku na ina akiba kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika, inayokadiriwa kuwa mapipa bilioni 48.4. Lakini sekta ya mafuta imekabiliwa na changamoto kubwa, hasa katika suala la usalama, huku nchi hiyo ikiendelea kugawanyika tangu uasi ulioungwa mkono na NATO ulipomwondoa madarakani na kumuua kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *