
Wafuasi 89 wa rais wa zamani wa mrengo wa kulia nchini Brazil, Jair Bolsonaro, wamejeruhiwa baada ya kupigawa na radi, walipokuwa wakiandamana kumuunga mkono rais wao huko Brasilia siku ya Jumapili, kulingana na wazimamoto.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika katika mji mkuu wa Brazil wakati wa mvua kubwa kumuunga mkono Bolsonaro, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa jaribio la mapinduzi na anashikiliwa katika gereza nje kidogo ya jiji.
Umati huo, uliokusanyika karibu na Uwanja wa Cruzeiro, ghafla ulipigwa na radi na kusikika kelele kubwa, kulingana na video iliyorushwa na vyombo vya habari vya ndani na kwenye mitandao ya kijamii. Wazimamoto wamesema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP kwamba waliwahudimia watu 89 katika eneo la tukio kufuatia tukio hilo. Kati ya hawa, 47 walilazwa hospitalini, wakiwemo 11 ambao “walihitaji huduma kubwa ya matibabu.”
Maandamano ya Jumapili yaliandaliwa na mtu mwenye ushawishi na mbunge Nikolas Ferreira ili kuomba “msamaha” kwa Jair Bolsonaro. Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 70 amefungwa katika gereza la Papuda huko Brasilia. Anasumbuliwa na matatizo makubwa ya kiafya, likiwemo shambulio la kisu mwaka 2018 wakati wa kampeni za uchaguzi, shambulio ambalo lilihitaji operesheni kadhaa kubwa za upasuaji.