Baada ya Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) pia imeondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Guinea siku ya Jumatano, Januari 28, 2026, kufuatia mapinduzi ya mwaka 2021 yaliyoongozwa na kundi la wanajeshi lililoongozwa na Mamadi Doumbouya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Mamadi Doumbouya, 41, anaongoza nchi hiyo tangu mapinduzi ya 2021 yaliyomng’oa madarakani Rais mteule Alpha Condé, ambayo yalisababisha ECOWAS kuweka mfululizo wa vikwazo dhidi ya Guinea. Alishinda ushindi mkubwa kwa 86.72% ya kura katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba 2025, baada ya kipindi cha mpito cha miaka minne, licha ya ahadi yake ya awali kwamba yeye wala mwanachama yeyote wa jeshi hilo hangegombea na kwamba madaraka yangerudishwa kwa raia.

Mnamo mwezi Februari 2024, ECOWAS ilikuwa tayari imepunguza vikwazo vya kiuchumi na kifedha. Kufuatia kufanikiwa kwa kura ya maoni ya kikatiba mnamo Septemba 21, 2025, na uchaguzi wa urais mnamo Desemba 28, 2025, shirika hili la Afrika Magharibi “linaondoa vikwazo vyote vilivyobaki dhidi ya Jamhuri ya Guinea na wale waliohusika” katika mapinduzi na “kuirudisha” nchi hiyo katika taasisi zake, kulingana na taarifa.

ECOWAS pia inampongeza Mamadi Doumbouya kwa kuchaguliwa kwake kama mkuu wa nchi. Baada ya kumpindua Alpha Condé, rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Guinea, Kanali Doumbouya, ambaye baadaye alijipandisha cheo hadi kuwa Jenerali, aliwanyamazisha wapinzani: vifungo, kusisitishwa kwa vyama vya siasa na vyombo vya habari, watu kutoweka, na kutekwa nyara kwa wakosoaji kumekuwa kukienea.

Katika taarifa yake, ECOWAS “inahimiza serikali kuongeza juhudi zake za kuimarisha demokrasia, utawala bora, na utawala wa sheria, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *