Wafanyabiashara mkoani Dodoma wameanza kunufaika na mafunzo ya Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) yanayolenga kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kikodi, kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza uwazi katika usimamizi wa kodi kupitia mifumo ya kidijitali.

Akifungua mafunzo hayo, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Hassan Mcha, amesema mfumo wa IDRAS umeboresha utoaji wa huduma kwa kuwezesha wafanyabiashara kupata taarifa za kikodi kwa wakati, kuwasilisha taarifa na kufanya mawasiliano na TRA kwa njia ya mtandao, sambamba na kujenga imani na kuhimiza ulipaji wa kodi kwa hiari.

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea walipa kodi uelewa wa matumizi sahihi ya mfumo huo ili kuongeza ufanisi, usalama wa taarifa za kodi na kuhimiza ulipaji wa kodi kwa hiari, jambo litakalosaidia kuboresha mazingira ya biashara na mapato ya serikali.

#azamtvupdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *