Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema: “Vita vya siku 12 viliiweka Iran katika nafasi maalum na ya kipekee ya nguvu, na nina uhakika kwamba Marekani haiwezi kukariri upumbavu wa huko nyuma.

Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Hassan Abutourabi-Fard, amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Swala ya Ijumaa katika musalla wa Tehran na kuongeza kuwa: Historia imesajili kwamba, Iran ni nembo ya nguvu na heshima, chimbuko la huruma, uadilifu, kusimama kidete na hekima ambayo si mhanga wa vita wala mwanzilishi wa vita; Iran ni mshindi katika vita na Marekani.

Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema, jeshi la Marekani na pengine jeshi la Israel lilikuwa tayari kutoa pigo la mwisho kwa hatua za moja kwa moja za kijeshi ikiwa maendeleo yatafikia hatua muhimu na kuunda mazingira ya ukosefu wa utulivu nchini Iran, hali ambayo wabunifu wa senario hii walitarajia ingesababisha kusambaratika Iran.

Hujjatul-Islam Sayyid Mohammad Hassan Abutourabi-Fard amesisitiza: “Vikosi vya jeshi vya nchi viko katika kiwango cha juu cha utayari na vimeshikilia kitufe cha kufyatulia risasi na ikiwa hesabu isiyo sahihi itatokea na upumbavu wa Marekani ukarudiwa, basi mhimili wa Marekani na Uzayuni utalengwa katika muda mfupi iwezekanavyo.”

Aidha amezungumzia hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika orodha ya makundi ya kigaidi na kubainisha kwamba, uamuzi huo unachukuliwa kuwa kitendo kisicho na mantiki na cha uchochezi kinachokwenda sambamba na sera za utawala wa Washington na Tel Aviv.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *