
Bashar Al-Natoor, mkuu wa idara ya mfumo wa Kiislam katika shirika la Fitch Ratings, anasema hatifungani za sukuk Afrika zimepanda hadi dola bilioni 3 mwaka 2025, kutoka dola milioni 112 million mwaka uliotangulia, zaidi ikiwa ni kutokana na kurudi kwa kiwangoi cha Misri cha dola bilioni 2.8 baada ya kutokuwepo kwa mwaka mzima. Kwa kulinganisha, mauzo ya hatifungani za kimataifa Afrika yamezidi dola bilioni 13 kwa nchini Nigeria, Afrika Kusini, na Kenya.
Hatifungani za Sukuk za 2026 zimezidi dola milioni 580, hasaa kutokana na dola milioni 500 za Benin ambao walikuwa wanauza kwa mara kwanza, Al-Natoor amesema.
Nigeria, ambayo imeuza hatifungani za sukuk kwa sarafu za nchi hiyo, ni miongoni mwa nchi ambazo zinaangazia uwezekano wa kuwa na mfumo wa fedha wa Kiislam unaotumia sarafu ya dola, huku Rais Bola Tinubu akitaka bunge liidhinishe mauzo ya hatifungani za sukuk kimataifa.
Senegal pia imesema inaangalia uwezekano wa masoko ya kitaifa na kimataifa ya sukuk.
Admassu Tadesse, rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo, anasema kutakuwa na faida kubwa kwa serikali kupata uwekezaji kutoka kwa mataifa ya Ghuba.
“Kuna hamu sana kwa wawekezaji kutoka mataifa ya Ghuba kuwekeza katika masoko yanayoibuka, hasa barani Afrika,” Tadesse alisema wakati wa majadiliano katika kikao.