Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema kuwa Sudan imekumbwa na mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi wa ndani duniani, huku takriban watu milioni 9.5 wakilazimika kuhaka makazi yao katika majimbo 18.

Kwa takriban miaka mitatu, watoto wa Sudan wamevumilia hali mbaya inayozidi kuongezeka kutokana na machafuko, wimbi la wakimbizi wa ndani, magonjwa na njaa.

Shirika la UNICEF limeeleza kuwa linaendelea kutoa huduma nchini Sudan kwa kushirikiana na washirika wake katika kutoa huduma za kuokoa maisha kwa watoto na familia zilizoathiriwa na vita, ikiwa ni pamoja na huduma ya afya na lishe, maji salama, msaada ya kisaikoliojia na elimu. 

Hata hivyo, UNICEF imetahadharisha kuwa mgogoro wa Sudan umeripotiwa kwa kiwango cha chini, jambo linalozuia taasisi mbalimbali za masuala ya kibinadamu kuchukua hatua. 

Shirika hilo limesisitiza kuwa watoto nchini Sudan wanabeba mzigo mzito zaidi wa vita na kusisitiza kuwa kuna udharura wa kurejeshwa amani na utulivu nchini humo haraka iwezekanavyo . 

Jeshi la Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) wanapigana vita tangu Aprili 15, 2023 ambapo wapatanishi wa kikanda na kimataifa wameshindwa kuhitimisha vita hivyo. Maelfu ya Wasudani wameuliwa na wengine wengi kujeruhiwa katika vita hivyo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *