Shirika la Habari la Taifa la Iran limeripoti likinukuu kauli hiyo ya Khamenei leo Jumapili wakati mvutano kati ya Tehran na Washington ukiendelea kuongezeka.

Kulingana na shirika hilo, Khamenei amesema Iran haitaanzisha vita, lakini itatoa “pigo kali” kwa yeyote atakayelishambulia taifa hilo, na kwamba vita hivyo havitakuwa vya upande mmoja bali vitakavyoihusisha kanda nzima.

Onyo hilo linakuja wakati manuari ya jeshi la Marekani, ikisindikizwa na meli nyingine kadhaa za kivita, zimepiga kambi katika Bahari ya Arabia.

Huku haya yakijiri, Iran inapanga kufanya mazoezi ya kijeshi leo Jumapili katika eneo la Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni ujia muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani. Marekani imeionya Tehran kuhusu luteka hiyo ikiitaka isiwe tishio kwa meli zake au biashara ya kimataifa.

Kwa upande mwingine, spika wa bunge la Iran, Mohammad Bagher Qalibaf, amesema nchi hiyo sasa inachukulia majeshi yote ya Umoja wa Ulaya kama makundi ya kigaidi. Hii ni baada ya Umoja wa Mataifa kuliorodhesha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran kuwa kundi la kigaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *