
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani.
Wakati huu tunakuletea Kipindi cha Tupike Kijapani ambapo tutapika pamoja chakula cha “Hosomaki” hii ni aina ya sushi inayopikwa kwa kuviringisha mwani huku ndani yake ukiwemo wali na viambato vingine.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Pia tutasoma ujumbe wako msikilizaji. Usikose kusikiliza!